Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Darubini zaelekea Tanzania kuangazia uhuru wa vyombo vya habari duniani

Darubini zaelekea Tanzania kuangazia uhuru wa vyombo vya habari duniani

Tarehe Tatu Mei kila mwaka ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, lengo likiwa ni kumulika mwelekeo wa vyombo hivyo iwe ni redio, magazeti au televisheni katika kubadili maisha ya wananchi ili duniani pawe pahala salama na bora zaidi kwa kila mkazi wake.

Hata hivyo mwaka huu kutokana na kuchipuka kwa mitandao ya kijamii katika kuhabarisha umma, teknolojia ya digitali nayoimemulikwa sanjari na nafasi ya wanawake kwenye vyombo hivyo, miaka 20 baada ya mkutano wa kimataifa wa wanawake wa Beijing. Nini kimefanyika? Kurunzi letu linaelekea nchini Tanzania na msimulizi wetu ni Assumpta Massoi.