Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Kikwete atumaini kuvumbua jinsi ya kuimarisha utayari wa jamii dhidi ya majanga ya afya.

Rais Kikwete atumaini kuvumbua jinsi ya kuimarisha utayari wa jamii dhidi ya majanga ya afya.

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa jopo la Umoja wa Mataifa la kusaka jinsi dunia inaweza kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kwa siku za usoni, amesema leo kwamba anatarajia kutoa mapendekezo juu ya mapungufu yaliyoonekana wakati wa kupambana na Ebola.

Akihojiwa na Priscilla Lecomte na Jospeh Msami wa idhaa hii, ameeleza kwamba wanachama wa jopo hilo baada ya kuzungumza na wataalam wa afya mjini New York, Marekani, watatembelea Geneva, Uswisi, ili kujadiliana na wadau wa shirika la afya ulimwenguni, WHO na mashirika mengine, halikadhalika watasafiri kwenda nchi zilizoathirika na Ebola.

Hapa Rais Kikwete anaanza kwa kuelezea jukumu la jopo hilo ambalo ripoti yake ya awali wataiwasilisha mwezi Septemba, ripoti ya mwisho ikitarajiwa mwisho wa mwaka huu.