Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi 14,000 wa Nigeria waliokuwa Niger warejea mpakani: OCHA

Wakimbizi 14,000 wa Nigeria waliokuwa Niger warejea mpakani: OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu linasema takribani raia  14,000 wa Nigeria waliokuwa wakimbizi nchini Niger wamewasili mpakani mwa Niger na Nigeria tangu Mei sita mwaka huu wakijaribu kurejea nyumbani kwao .

Wakimbizi hao walichukuliwa na kuhifadhiwa katika kambi ya muda huko Geidam jimboni Yobu nchini Nigeria .

OCHA inasema wengi wa  wakimbizi wanaorejea makwao ambao ni wavuvi na wafanyabiashara wameishi ziwani Chad kwa zaidi ya miongo mitatu na haijajulikana idadi kamili ya wale ambao hawajarejea. Jumuiya ya usaidizi wa kibinadamu inataka pande zilizoathiriwa na kundi la kigaidi la Boko Haram kuhakikishiwa  ulinzi na usaidizi

Raia wengi wa  Nigeria wamelazimika kukimbilia ziwa Chad nchini Niger kutokana na vitendo vya kikatli vinavyotekelezwa na Boko Haram.