Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya vikao vya faragha Rais Kikwete aelezea mwelekeo wa jopo lao

Baada ya vikao vya faragha Rais Kikwete aelezea mwelekeo wa jopo lao

Mwenyekiti wa jopo la Umoja wa Mataifa la kusaka jinsi dunia inaweza kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kwa siku za usoni, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania leo amezungumza na waandishi wa habari mjini New York na kuelezea mwelekeo wa jukumu lao wakati huu ambapo magonjwa ya milipuko yanatishia amani na ustawi katika baadhi ya nchi duniani. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Jopo hilo la watu sita likiongozwa na Rais Kikwete limekuwa na vikao vya kwanza kabisa vya faragha kwa takribani siku nne ambapo leo mwenyekiti huyo ametoa muhtasari kwa wawakilishi wa nchi wanachama kwenye Umoja wa mataifa na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari.

(Sauti ya Kikwete)

Ripoti kamili ya jopo hilo itawasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi Disemba mwaka huu na hatimaye Katibu Mkuu ataiwasilisha Baraza Kuu.

(Sauti ya Kikwete)