Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jopo kutathmini masuala ya afya laanza kazi yake

Jopo kutathmini masuala ya afya laanza kazi yake

Jopo lililoundwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kusaka jinsi dunia inaweza kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kwa siku za usoni, limehitimisha mkutano wake wa kwanza jijini New York chini ya mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania. Maelezo zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Vikao vya jopo hilo lenye watu Sita akiwemo mwenyekiti wake Rais Kikwete vimekuwa vya faragha kuanzia Jumanne wiki hii ambapo leo Ijumaa mwenyekiti huyo aliwapatia muhtasari wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa jijini New York.

Muhtasari huo pia ulitolewa faraghani ambapo idhaa hii iliweza kuzungumza na Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ramadhani Muomba Mwinyi juu ya yanayojiri.

(sauti ya balozi Mwinyi)

 Halikadhalika akazungumzia nafasi ya Afrika kwenye jopo hilo.

(sauti ya balozi Mwinyi)