Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusitokomeze waliyopigania mashujaa wa vita kuu ya pili ya dunia:Ban

Tusitokomeze waliyopigania mashujaa wa vita kuu ya pili ya dunia:Ban

Kumbukizi ya kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia zimeendelea huko barani Ulaya ambako hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshiriki tukio la aina hiyo mjini Kiev nchini Ukraine.Taarifa kamili na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Tukio hilo limefanyika kwenye eneo la kuwakumbuka askari na raia wa Ukraine waliopigana kulinda nchi yao dhidi ya utawala wa manazi ambapo Ban amesema anahisi hisia za mashujaa za kuona wananchi wa Ukraine wakiishi kwa amani huku wakilinda mamlaka za taifa lao.

Akiwa na mwenyeji wake Rais Petro Poroshenko wa Ukraine, Ban amesema..

(Sauti ya Ban)

"Ukraine imechangia  kwa kiasi kikubwa na kujitoa mhanga, ukweli ambao ulimwengu hauwezi kusahau kamwe. Na t ukikumbuka yale waliyoyapitia ili kupata ushindi dhidi ya ufashisti, sisi tunatoa ahadi mpya kwamba vifo vyao havitakuwa bure. Ni kwa ajili ya janga hili ndio jumuiya ya kimataifa ilikuja pamoja na kuunda Umoja wa Mataifa. Mkataba wa Umoja wa Mataifa anasema lengo lao kuu ni "kuokoa vizazi vijavyo kutoka na janga la vita."

Amesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa zitaendelea kushikamana na wananchi wa Ukraine huku akielezea kuvutiwa kwake na uongozi na dira ya Rais Poroshenko, katika kusimamia uhuru na mamlaka za Ukraine.