Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini Poland, Ban akumbuka mateso ya vita vikuu vya pili miaka 70 iliyopita

Nchini Poland, Ban akumbuka mateso ya vita vikuu vya pili miaka 70 iliyopita

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kwamba kumbukizi ya mateso ya vita vikuu vya pili vya dunia ni fursa ya kukumbuka umuhimu wa kutunza maadili ya Umoja wa Mataifa.

Amesema hayo alipohudhuria kumbukizi hiyo ya miaka 70 baada ya kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia , mjini Gdansk, nchini Poland.

Bwana Ban ameongeza kwamba Umoja wa Mataifa umeundwa miaka 70 iliyopita baada tu ya vita hivyo ambavyo vilikuwa ni wakati wa uhalifu unaozidi, ukosefu wa imani na utu, na ambapo mamilioni ya raia walipoteza maisha, hasa vijana.

Ameongeza kwamba masharti mengi ya sheria ya kimataifa yametokana na masomo ya vita vikuu vya pili.

Kwa hiyo vita hivi vikuu vya pili vya dunia vimetuletea mifumo muhimu sana, mamlaka za kisheria na kisiasa, na watu wameamua kwamba hatupaswi kurudia tena makosa kama hayo. Lakini kwa bahati mbaya, wakati mkataba wa Umoja wa Mataifa ukikariri kuwa tutaepusha viazi vijavyo na janga la vita, bado tunaona mizozo na mauaji ya watu hapa na pale

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameisihi jamii ya kimataifa kuheshimu maadili ya Umoja wa Mataifa, ikiwemo kutoshambuliana, kutatua mizozo kwa amani na kuheshimu haki za binadamu.