UNRWA, Brazil zakuza ushirikiano

7 Mei 2015

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA Pierre Krähenbühl ametumia ziara yake ya kwanza rasmi nchini Brazil kuelezea umuhimu wa kukuwa kwa ushirikiano kati ya shirika hilo na mataifa ya Amerika ya Kusini.

Katika ziara yake amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Brazil, wabunge na wadua wengine muhimu nchini humo.

Kadhalika mkuu huyo wa UNRWA amekutana na kiongozi wa haki za binadamu mau wa mji wa Sao Paulo na wawakilishi wa taasisi binafsi.

Akiwa nchini humo Bwana Krähenbühl amezindua makataba ya picha ya UNRWA iitwayo safari ndefu katiak makumbushoa ya taifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter