Mkuu wa MINUSCA apata matumaini na kongamano la Bangui

Mkuu wa MINUSCA apata matumaini na kongamano la Bangui

Wakati kongamano la amani na maridhiano la Bangui likiendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini humo Babacar Gaye ameelezea matumaini yake kuhusu mwelekeo nchini kote. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Akihojiwa na redio ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSCA, Jenerali Babacar Gaye amesema kongamano hilo ni ukomo wa utaratibu mrefu wa kufikia maridhiano, akiwaambia raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwamba matumaini ya amani yapo kupitia kongamano hilo llililoanza jumatatu kwenye makao makuu ya serikali ya mpito, na ihudhuriwa na rais wa serikali ya mpito Catherine Samba-Panza, viongozi wa kisiasa, we serikali za mitaa na wa dini na wawakilishi wa jamii ya kimataifa na nchi jirani akiwemo rais wa Congo, Denis Sassou-Nguesso.

(SAUTI GAYE)

« Kwa mara ya kwanza, raia wanawakilishwa na watu ambao wametoka kwenye jamii, ambao watajaribu kupaza sauti zao ili shida zao zisikike kwenye kongamano hilo ambalo tunadhani ni fursa ya kuunda upya Jamhuri ya Afrika ya Kati »

Mada nne ambazo ni Haki na Maridhiano, Utawala, Amani na Usalama na Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii zitazungumza kwenye kongamano hilo linalotakiwa kumalizika tarehe 11 mwezi huu.