Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yazindua kituo cha ugunduzi na uwezeshaji kifedha

UNICEF yazindua kituo cha ugunduzi na uwezeshaji kifedha

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF leo  limezindua kituo kipya cha kimataifa cha ugunduzi na fedha kwa ajili ya kukuza mipango ya miradi inayopunguza ukosefu wa usawa ,  kuongeza ubunifu na kupunguza gharama kwa ajili ya maisha bora ya watoto masikini.

Taarifa ya UNICEF inasema hadi sasa kiasi cha dola za Marekani milioni tisa zimechangishwa ili kusaidia kituo hicho kitakachowezesha timu ya kituo cha zamani chenye miaka saba kuanzisha miakati mipya ya kuoboresha maisha ya watoto katika maeneo masikini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Anthony Lake, ugunduzi wa kuitumia teknolojia zinazohamishika kusajili vizazi vipya, kushirikishana taarifa za kuboresha elimu, afya na kuwapa vijana njia  ya kuunganishwa na seriakali zao vimeanza kubadilisha namna ya kufanya kazi .

Mkuu huyo wa UNICEF amefafanua kuwa hatua hizi kwa sasa sio mawazo pekee bali ni mambo ambayo yanatokea na kusaidia kuchochea mabadiliko kwa watoto walio katika mahitaji makubwa na kuongeza kuwa hata hivyo ugunduzi zaidi unahitajika kw adharura.