Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumejizatiti kutokomeza mauaji ya Albino:Tanzania

Tumejizatiti kutokomeza mauaji ya Albino:Tanzania

Wakati juhudi za kimataifa za kukabiliana na mauajai dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino zikichukua kasi  Tanzania moja ya nchi inatotajwa kukithiri katika mauaji hayo imesema licha ya elimu dhidi ya dhana potofu ya utajiri kupitia viungo vya albino inachukua hatua nyingine anuai .

Katika mahojiano maalum kwa njia ya simu na idhaa hii Waziri Mkuu wa Tanzania  Mizengo Pinda amesema katika kutokomeza mauaji dhidi ya albino mipango ya muda mfupi na muda mrefu inahitajika na kwa sasa.

(SAUTUI PINDA)

Hivi karibuni ofisi y a Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu ilipendekeza mikakati ya kukabiliana na mauajia ya albino ikiwamo elimu kwa umma, kuimarisha ulinzi wa kijamii na  kuongeza polisi kwenye wilaya zenye matukio mengi zaidi.