Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Mihadarati imepata rais mpya:

Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Mihadarati imepata rais mpya:

Bodi ya kimataifa ya kudhibitio mihadarati (INCB) inayoendelea na kikao chake cha 113 imemchagua Bwana Werner Sipp kuwa Rais wake mpya. Rais huyo wa Ujerumani , Bwana Sipp alijiunga na INCB mwaka 2012 baada ya uzoefu wa muda mrefu katika Nyanja ya taifa na kimataifa ya sera za kudhibiti mihadarati na ushauri wa kisheria.

Amewahi kuwa mtaalamu mshauri kwenye wizara ya afya ya shirikisho la Ujerumani, jumuiya ya Ujerumani ya ushirikiano wa kimataifa na katika miradi mbalimbali ya Muungano wa Ulaya ikiwemo baraza la Ulaya, na mwandishi wa kisheria wa Ujerumani katika takwimu za kisheria kuhusu mihadarati barani Ulaya.

Baada ya kuchaguliwa Bwana Sipp amesema katika miezi ijayo kuelekea kikao maalumu cha baraza kuu kuhusu matatizo ya mihadarati duniani hapo April 2016, jumuiya ya kimataifa ni lazima ikabiliane na changamoto nyingi kama kuchagiza afya na ustawi wa watu kwa kuwalinda na kuathirika na dawa za kulevya , lakini pia inatakiwa kudhibiti uzalishaji na usafirishaji haramu wa mihadarati na hatari zinazosababishwa na mihadarati hiyo kote duniani.

Bodi pia imechakuwa wajumbe wapya ambao watakuwa wanamsaidia Rais kutekeleza malengo atakayokuwa ameyaainisha.