Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wahamishwa kutoka kisiwa cha ziwa Chad:OCHA

Maelfu wahamishwa kutoka kisiwa cha ziwa Chad:OCHA

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema makadirio ya awali kutoka serikali ya Niger yanaonyesha kuwa watu 25,000 wamewasili Nguigmi na Bosso  mashariki mwa Niger tangu tarehe 30 April.

Watu hao waliambiwa kuondoka kisiwani ziwa Chad kutokana na mipango ya operesheni za kijeshi pa muungano wa majeshi ya Chad, Niger na Nigeria dhidi ya kundi la Boko Haram.

OCHA inasema karibu Wanaigeria 5,000 wamewasili Diffa kutoka kisiwani humo mnamo Mai 3 na wengi wao walikuwa njiani kurejea Nigeria umesema uongozi wa eneo hilo.

Kuwasili kwa waziri mkuu, maafisa wa serikali watoa huduma za kijamii kwa watu waliotawanywa huko Nguigmi hapo jana Mai 5 wamebaini kuwa wengi wa watu hao wanahitaji haraka maji, chakula na malazi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa lita 10,000 za maji kwa familia, wakati ambapo lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatoa msaada wa vifaa vya nyumbani kwa watu 5000 huku la idadi ya watu duniani UNFPA na lile la afya WHO wanasaidia vifaa na huduma za afya.