UNDP, wasaini makubaliano ya kuinua uchumi jimboni Basra
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na mamlaka ya jimbo la Basra nchini Iraq, leo wamesaini makubaliano yanayolenga katika kuimarisha ushiriki na uwajibikaji wa serikali na kuhuisha shughuli za kiuchumi katika jimbo hilo la kusini mwa nchi hiyo.Kwa mujibu wa taarifa kuhusu makubaliano hayo, mpango huo pia unahusisha kulinda utamaduni na mazingira ya kisiwa cha Mesopotamian Marshlands.
Taarifa hiyo inafafanua kuwa utajiri wa mafuta sio pekee lengo la ushirikiano bali pia uwekezaji katika uwezo wa watu na maendeleo ya sekta binafsi.
Makubaliano hayo kadhalika yanaainisha ushirikiano katika siku za usoni katika maeneo kama vile ugatuzi, menejimenti ya fedha, ulinzi wa mazingira, maendeloe kupitia sekta binafsi pamoja na mkakati wa miaka mitano wa kuwezesha jimbo la Basra.