Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNISDR yaipongeza Geneva kwa kudhibiti mafuriko:

UNISDR yaipongeza Geneva kwa kudhibiti mafuriko:

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza hatari ya majanga, UNISDR,  Margareta Wahlström, leo Jumatano ameupongeza mji wa Geneva kwa jinsi ilivyofanikiwa kudhibiti mafuriko yaliyokuwa yanatishia mji huo katika siku za karibuni kufuatia mvua kubwa inayonyesha kwenye milima ya French Alps.

Geneva ni maskani ya UNISDR na mashirika mengine 40 ya Umoja wa mataifa. Mlima Arve unaoungana na mlima Rhone mjini Geneva uliongeza kufurika kutoka mita 90 kwa dakika hadi mita 900 kwa dakika na hivyo kuweka wahudumu wa dharura katika tahadhari na kulazimika kuwahamisha watu na pia kufunga barabara.

Ingawa kumekuwepo na usumbufu kiasi lakini kwa ujumla hatari ya janga imepunguzwa kutokana na ukarabati na udhibiti wa mifumo ya mito na maziwa kwa nchi zote mbili za Uswis na Ufaransa.

Bi. Wahlström amesema ni vizuri kujua kwamba mji ambao ni mwenyeji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Geneva na mashirika mengine makubwa ya Umoja wa Mataifa unaweza kuchukuliwa kama mfano wa kuigwa linapokuja suala la udhibiti wa mafuriko.

Ameongeza kuwa mafuriko yanaathiri watu wengi zaidi ya majanga ya aina nyingine na yanahitaji kudhibitiwa vilivyo kuepuka kupoteza maisha ya watu wengi zaidi na athari za kiuchumi.