Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wahaha kusaka suluhu ya mgogoro Burundi

Umoja wa Mataifa wahaha kusaka suluhu ya mgogoro Burundi

Umoja wa Mataifa unahaha kunusuru  hali ya machafuko nchini Burundi baada ya mahakama ya katiba nchini humo kumruhusu rasmi Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza kugombea tena nafasi hiyo kwa awamu ya tatu hatau iliyochochea zaidi maandamano nchioni humo.Msemaji wa ujumbe wa Umoaj wa Mataifa wa uangalizi wa uchaguzi  MENUB,  Vladinir Monteiro,  ameiambia redio ya Umoja wa Mataifa kuwa juhudi za upatanishi zinaendela ambapo wadau muhimu kama vile wawakilishi wa serikali, upinzani, asasi za kiraia na viongozi wa  dini wamekutanishwa katika kusaka suluhu na kusisitiza

(SAUTI MONTEIRO)

Mwitikio wa Katibu Mkuu ni kile kilichosemwa na msemaji wake hivi karibuni ,kuitaka Burundi  kulinda amani waliyoisaka kwa muda mrefu  na kutatua tfauti zao kwa majadiliano.