Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio lapitishwa kuhusu ushirikiano kati ya UM na taasisi za kikanda

Azimio lapitishwa kuhusu ushirikiano kati ya UM na taasisi za kikanda

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa amekaribisha hatua kupitishwa kwa azimio la kisiasa kuhusu uimarishaji wa ushirikiano kati ya umoja huo na taasisi za kikanda na maeneo.

Katika hotuba yake baada ya azimio hilo kupitishwa kwa kauli moja, Kutesa amesema ni ishara ya nia ya nchi wanachama kusongesha mbele ushirikiano wa kimkakati na Umoja wa Mataifa.

Amewashukuru wajumbe kwa mijadala ya dhati iliyowezesha kuibuka na azimio hilo ambalo pamoja na mambo mengine linasisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya vyombo  hivyo katika masuala ya amani, ulinzi, maendeleo na haki za binadamu.

Halikadhalika azimio hilo linataka kuimarishwa kwa ubia wa kimkakati unaoendeleza misingi ya kunufaika na fursa ambayo nchi ina uwezo nayo zaidi na usaidizi.

Bwana Kutesa amesema azimio hilo limepitishwa wakati muafaka ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ziko kwenye harakati za kuhitimisha ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015