Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timu za ukozi zajiandaa kuondoka Nepal:OCHA

Timu za ukozi zajiandaa kuondoka Nepal:OCHA

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, limesema wakati timu za utafutaji na uokozi zikijiandaa kuondoka nchini Nepal awamu inayofuata ya ufikishaji misaada inayohitajika haraka inashika kasi.

OCHA inasema ili kuhakikisha uratibu wa misaada hiyo karibu na watu walioathirika Zaidi na tetemeko la mwezi uliopita vituo maalumu vimeanzishwa Gorkha na Sindhupalchowk ambako tathimini inaonyesha kwamba asilimia 80 na 90 ya nyumba zimebomolewa na familia zinahitaji haraka malazi, chakula na madawa.

Vituo hivyo vya uratibu wa misaada pia vimeanzishwa katika wilaya zingine tano kusaidia ufikishaji na usambazaji wa misaada.