Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wakumbuka wahanga wa vita kuu ya pili ya dunia

Umoja wa Mataifa wakumbuka wahanga wa vita kuu ya pili ya dunia

Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kumefanyika hafla maalum ya kumbukizi ya wahanga wa vita vikuu ya pili ya dunia miaka 70 iliyopita. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Katika tukio hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepanda mti mbele ya jengo la Baraza Kuu kwa ajili ya mamilioni ya raia waliokufa wakati wa vita hivyo wakiwemo mamilioni ya wayahudi waliouawa kwa sababu ya kabila lao.

Ban amesema tukio hilo ni ni njia ya kukumbuka maadili ya Umoja wa Mataifa ambayo yaliundwa wakati ule, yaani miaka 70 iliyopita, ili kuzuia uhalifu kama huu usitokee tena.

Naye katika hotuba yake rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa amesema kwamba jamii inapaswa kukumbhuka kwamba Umoja wa Mataifa umeundwa ili kuhakikisha uwepo wa umoja na amani baina ya mataifa.

Bwana Kutesa amekumbusha pia wajibu wa jamii ya kimataifa katika kuzuia vita na kulinda haki za binadamu.

Vita vikuu vya pili vilianza mwaka 1939 hadi Mei 1945. Mkataba wa Umoja wa Mataifa ulisainiwa na mataifa 51 tarehe 26, Juni, mwaka