Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR kuzindia tovuti maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi

OHCHR kuzindia tovuti maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa leo inazindua tovuti maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi au albino.Tovuti hiyo itakayoitwa “Watu wenye ulemavu wa ngozi :sio mashetani bali binadamu” ni maalumu kushughulikia masuala yanayohusu ulemavu wa ngozi na itatoa fursa ya kufahamu masuala mbalimbali kuhusu hali hiyo ambayo bado haieleweki vizuri kijamii na kiafya.

Ravina Shamdasani ambaye ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu amesema tovuti inaelezea masuala muhimu ya haki za binadamu ambayo yanawakabili  kila siku watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na hadithi za mashujaa 12 ambao ni watu wenye ulemavu wa ngozi na wasio na ulemavu wa ngozi ambao wanafanya kazi kuleta mabadiliko.