Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF kusaidia familia zilizokimbia kambi ya Yarmouk:

UNICEF kusaidia familia zilizokimbia kambi ya Yarmouk:

Katika kulisaidia shirika la Umoja wa mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA , shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wiki hii nlimeshiriki katika safari mbili zilizohusisha mashirika mengine pia ili kutoa msaada wa kibinadamu kwa familia ambazo zimetawanywa kutoka katika kambi ya Yarmouk.

Familia nyingi zimetawanywa katika maeneo matatu , Yalda, Babila na Beit Saham ambako ni kilometa 10 kutoka mji mkuu wa Syria Damascus. Hii ni mara ya kwanza UNICEF imeweza kupata fursa ya kufika maeneo hayo kwa miaka miwili iliyopita.

Baada ya kupita vizuizi vitano vya barabarani UNICEF imeweza kufikisha malori matatu yaliyosheheni nepi 9000, vifaa 15000 vya watoto wachanga na jozi 2800 za nguo za watoto.