Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa MONUSCO alaani mashambulizi dhidi ya helikopta Beni

Mkuu wa MONUSCO alaani mashambulizi dhidi ya helikopta Beni

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, Martin Kobler, amelaani vikali mashambulizi yaliyofanyika dhidi ya helikopta ya MONUSCO kwenye eneo la Beni.

Mashambulizi hayo yametokea asubuhi ya jumatatu hii, kilomita 20 kutoka Beni. Helikopta imepigwa risasi na kundi la wanamgambo wasiojulikana na ikatua kwa usalama.

Bwana Kobler amesema mashambulizi hayo dhidi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa hayakubaliki na hayavumiliki, akiongeza kwamba MONUSCO haitazuiliwa kulinda raia.

Aidha amesema watekelezaji wa mashambulizi hayo watatafutwa na jitihada zote.