Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sitisheni mashambulizi ya anga kwenye uwanja wa ndege Sana’a: OCHA

Sitisheni mashambulizi ya anga kwenye uwanja wa ndege Sana’a: OCHA

Mratibu wa ofisi ya usaidizi wa kibinadamu, OCHA nchini Yemen Johannes Van der Klaaw amesihi washirika kwenye mashambulizi ya anga nchini humo wasitishe harakati zao kwenye uwanja wa ndege Sana’a ili huduma za kibinadamu kwa wahitaji ziweze kuendelea.

Bwana der Klaaw ambaye amenukuliwa katika taarifa akisema wiki iliyopita mashambulizi kutoka angani yamekuwa yakilenga uwanja  huo wa ndege na hivyo hakuna ndege iliyoweza kutua au kupaa wakati njia ya ndege inafanyiwa ukarabati.

Amesema viwanja vya ndege vya Yemen na bandari ni muhimu zaidi hivi sasa kwa mustakhbali wa nchi hiyo kwa kuwa bila kuweza kuvitumia hakuna wafanyakazi wa misaada au shehena za misaada ikiwemo dawa zinaweza kuingizwa nchini humo.