Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za kemikali za kielektroniki zaangaziwa:UNEP

Athari za kemikali za kielektroniki zaangaziwa:UNEP

Nchi 180 wanachama wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP zimeanza mkutano wao huko Geneva, Uswisi lengo ni kuandaa makubaliano ya kupunguza kemikali hatarishi zitokanazo na taka za kielektroniki kama vile kompyuta, microwave na simu.

UNEP inasema kwa sasa kuna aina Laki Moja za kemikali zinazotambuliwa ulimwenguni kutokana na bidhaa hizo lakini kiwango cha madhara yake kwa  binadamu bado hakiko dhahiri.

Inaelezwa kuwa kemikali hizo husababisha vifo vya watu zaidi ya Milioni Moja kila mwaka duniani kote na watu hao hukumbwa na madhila hayo wakati wanashika au kushughlikia kemikali hizo ikiwemo zile zitokanazo na taka za vifaa vya kieletroniki ikiwemo kompyuta na simu.

Mkurungezi mtendaji wa UNEP Achim Steiner anasema katika zama za sasa mtu mmoja anaweza kuwa na simu za mkononi au kompyuta zaidi ya moja na hatimaye anapovichoka  utupaji wake ni mashaka na kuleta athari hivyo…

 “Kemikali zinazoharibu mfumo wa tezi kama vile zebaki, hukanganya homoni na hata kujifananisha nazo, na hivyo kuwa na athari kubwa kwenye miili yetu, athari ambazo zinaweza kuharibu kwa kiasi kikubwa viungo vya ndani, uwezo wa ufahamu na hata afya kwa ujumla.”

Lengo la mazungumzo hayo hatimaye ni kuboresha mikataba mitatu ya kimataifa ambayo inahusika na uhuishaji wa kemikali za kielektroniki ambazo UNEP inasema mwaka jana pekee zilikuwa tani Milioni 41 nukta Nane