Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heko Sudan Kusini kwa kuridhia CRC

Heko Sudan Kusini kwa kuridhia CRC

Sudan Kusini imekuwa nchi ya 195 kuridhia mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto, CRC kitendo ambacho kimepongezwa na kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za mtoto.

Kufuatia hatua hiyo, kamati hiyo imetoa wito kwa Somalia na Marekani kufanya hima kuridhia mkataba huo unaoelezwa kuwa ndio mkataba wa haki ulioridhiwa na nchi nyingi zaidi duniani.

Taarifa ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imenukuu kamati hiyo ikizitaka Sudan Kusini na nchi zote zilizoridhia mkataba huo kuchukua hatua zaidi na kutekeleza ikiwemo kutunga sheria zinazozingatia misingi ya mkataba huo.

Mkataba huo ulioanza kutumika miaka 25 iliyopita umetaja misingi mikuu minne ya haki za mtoto ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kulindwa na kushirikishwa.