Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzoefu wetu Kenya umetufunza mengi licha ya changamoto: Guyo

Uzoefu wetu Kenya umetufunza mengi licha ya changamoto: Guyo

Kila uchao mizozo yenye misingi ya misimamo mikali ya kidini inaibuka maeneo mbali mbali duniani na kusababisha majanga ikiwemo vifo. Harakati mbali zimekuwa zinachukuliwa ili kushughulikia n a hata kuepusha ghasia hizo kwa mustakhbali wa wakazi wote wa dunia hii.

Syria, Mali, Iraq, Libya dunia inashuhudia majanga na ndio maana hivi karibuni huko Morocco, taasisi ya mfalme Abdulla wa pili, KAICIID kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa waliandaa mkutano wa siku mbili kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika kuzuia uchochezi unaoweza kusababisha vitendo vya ukatili. Miongoni mwa walioshiriki ni Guyo Liban Dadacha mjumbe wa Tume ya Taifa ya uwiano na maridhiano nchini Kenya.

Katika mahojiano yaliyowezeshwa na Madiha Sultan wa Radio ya Umoja wa Mataifa na kukamilishwa na Grace Kaneiya wa Idhaa hii, Guyo alielezea mambo kadhaa ikiwemo ushiriki wake kwenye mkutano huo uliofanyika Fez.