Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya amani ya Syria kuanza tena Geneva jumatatu

Mazungumzo ya amani ya Syria kuanza tena Geneva jumatatu

Majadiliano kuhusu Syria yataanza tena kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyopo mjini Geneva, Uswisi jumatatu, tarehe 4, Mei kwa kipindi cha wiki kati ya tano hadi sita.

Mjumbe Maalum wa Katibu mkuu nchini Syria, Steffan de Mistura, amewaita wawakilishi wengi kutoka kwa pande za serikali, upinzani na jamii, pamoja na wadau wengine wa kikanda na kimataifa kushiriki mjadala huo.

Wadau hawa wanatakiwa kueleza maoni yao kuhusu hali nchini humo, na mazungumzo ya moja kwa moja na ya pamoja yataratibiwa na Mjumbe maalum na Msadizi wake Ramzy Ezzeldine Ramzy.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kwamba wakati wa mazungumzo hayo, washiriki hawatajieleza mbele ya waandishi wa habari wala kuchukuliwa picha.