Hali ya utulivu imerejea Kass, Darfur baada ya makabiliano:UNAMID

1 Mei 2015

Kamanda mkuu wa vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur nchini Sudan, UNAMID Luteni Jenerali Paul Mella amesema hakuna tena wananchi waliozingira kituo ujumbe huo huko Kass kufuatia makabiliano ya hivi karibuni kati ya walinda amani na watu wasiojulikana yaliyosababisha majeruhi miongoni mwa walinda amani na vifo vya washambuliaji.

Akihojiwa na Idhaa hii baada ya ziara yake kwenye eneo hilo Luteni Jenerali Mella amesema wananchi hao walikuwa wanadai fidia ya vifo vilivyotokea lakini waliweza kuondoka baada ya..

(Sauti Mella-1)

Ili kubaini ukweli halisi wa tukio hilo na waliouawa pande mbili hizo zimekubaliana kuanza uchunguzi ambao Mkuu huyo wa UNAMID anasema..

(Sauti Mella-2)

Kambi ya Kass ni mojawapo ya kambi 36 za UNAMID nchini Sudan.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter