Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanahabari waachwe watekeleze wajibu wao:Kutesa

Wanahabari waachwe watekeleze wajibu wao:Kutesa

Kuelekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari May 3 , tukio maalum la kuadhimisha siku hiyo limefanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York chini ya kauli mbiu Ruhusu Ustawi wa Vyombo vya Habari, katika kuripoti usawa wa kijinsia , usalama wa vyombo vya habari katika kizazi cha dijitali.

Katika tukio hilo lililowaleta wadau wa vyombo vya habari na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu , Sayansi na Utamaduni(UNESCO), Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa ameelezea kusikitishwa na vifo na mateso wanayokumbana nayo wanahabari wakati wakiwa kazini na kusisitiza umuhimu wa tasnia hiyo.

(SAUTI KUTESA)

"Tukiwa katika mazingira yetu salama ya nyumbani au makazini twaweza kujifunza matukio muhimu duniani ikiwamo yale ya gizani. Wanahabari wanaziba pengo la taarifa katika kazi zao, tunajifunza kuhusu ugunduzi, bila wao tusingefahamu kuhusu maendeleo. Pia tusingesikia vilio vinavyonyamazishwa, ukiukwaji au maisha yanayodhulumiwa. "

Wanahabari zaidi ya 60 kote duniani waliuwawa mwaka jana wakitekeleza wajibu wao huku mwaka huu hadi sasa takribani wanahabari 40 wamepoteza maisha.