Ukanda wa Asia-Pacifiki kinara wa ukuaji wa uchumi

Ukanda wa Asia-Pacifiki kinara wa ukuaji wa uchumi

Ukanda wa Asia Pacifiki umekuwa kiongozi katika ukuaji wa uchumi wa dunia, na utazidi kuwa chanzo cha ukuaji katika siku za usoni, amesema Shamsad Akhtar, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Kamisheni ya Kiuchumi na Kijamii ya Umoja wa Mataifa kwa Asia na Pacifiki (ESCAP).

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mkutano wa juu kuhusu fedha kwa maendeleo endelevu ulioanza mjini Jakarta, nchini Indonesia, jumatano hii, unaokusanya wawakilishi 200 kutoka nchi 40, wakiwemo mawaziri 50.

(SAUTI SHAMSAD)

« Kinachotia matumaini kutoka kwa ukanda wetu ni uzoefu wetu mkubwa na wa aina mbalimbali kuhusu mafanikio na kasoro kwenye sekta ya fedha. Uzoefu wa ukanda wetu kama soko linaloibuka na linaloongoza  unaionyesha dunia mwelekeo kuhusu maendeleo »

Bi Akhtar ameongeza kwamba, bila kubuni nyenzo mbadala kwa kufadhili maendeleo, ikiwemo kupitia kipato cha ndani cha nchi, malengo ya maendeleo endelevu ya baada ya mwaka 2015 yataweza hatatatimizwa.

Lendo la mkutano huo wa Jakarta ni kukamislisha maandalizi ya kongamano la tatu la kimataifa kuhusu Fedha kwa Maendeleo litakalofanyika nchini Ethiopia mwezi wa Julai.