Asbestos bado ni tishio barani Ulaya:WHO
Shirika la afya duniani WHO limesema theluthi moja ya watu milioni 900 barani Ulaya wanaishi katika nchi ambazo bado hazijapiga marufuku mifumo yote ya asbestos, na hii inawaweka katika hatari iwe kazini au katika mazingira.
Shirika hilo linasema katika nchi ambazo zimeshapiga marufuku hatari iliyopo ni ya matumizi ya siku za nyuma. Limeongeza kuwa kufanyakazi au kuishi katika mazingira yenye asbestos kunaweza kusababisha saratani ya mapafu, mirija ya uzazi au ovari na zoloto na methothelioma. Na njia bora ya kutokomeza maradhi haya ni kuacha kutumia ain azote za asbestos.
Hayo yamesemwa katika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mazingira na afya unaofanyika Haifa Israel, ambao umetoa wito kwa nchi za Ulaya kutokomeza magonjwa yanayosababishwa na mifumo ya asbestos.
Wawakilishi zaidi ya 200 kutoka nchi za Ulaya na mashirika ya kimataifa nay a kitaifa yasiyo ya kiserikali yamehudhuria mkutano huo uliokuwa unatathimini hatua za kiafya na mazingira barani Ulaya.