UNESCO yaadhimisha muziki wa jazz duniani kote

30 Aprili 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa Ban Ki-moon anaendelea leo na ziara yake Ufaransa ambapo atazungumza na waziri wa mambo ya nje Laurent Fabius na kuhudhuira maadhimisho ya siku ya kimataifa ya jazz. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Huu ni muziki wa jazz kutoka Ethiopia katika maadhimisho ya siku ya jazz duniani yaliyofanyika mapema, katika siku chache zilizopita.

Kwenye ujumbe wake kwa siku hii, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, Irina Bokova amesema jazz ni muziki wa amani kwani ni mchanganyiko wa mitindo kutoka maeneo mbalimbali ya dunia.

“Tunahitaji hamasa ya Jazz (the spirit of jazz) zaidi leo ili kuleta watu pamoja, hasa vijana na wasichana, ili kukuza uhuru na amani na kupambana na aina mpya za chuki”

Sheree za kuadhimisha siku ya kimataifa ya muziki za jazz zinafanyika leo kwenye makao makuu ya UNESCO mjini Paris na katika nchi 185, ikiwemo Tanzania na Kenya.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter