Skip to main content

Nitazungumza na Rais Mteule Buhari kuhusu hatma ya watoto wanaoshikiliwa: Mjumbe UM

Nitazungumza na Rais Mteule Buhari kuhusu hatma ya watoto wanaoshikiliwa: Mjumbe UM

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu elimu duniani, Gordon Brown amekaribisha kuachiliwa huru kwa wasichana 200 waliokuwa wanashikiliwa na kikundi cha kigaidi cha Boko Haram nchini Nigeria huku akitaka wanaosalia waachiliwe huru mara moja.

Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq akizungumza na waandishi wa habari amemnukuu Bwana Brown akisema wakati umefika kumaliza jinamizi linalokabili wasichana ambao bado wako mikononi mwa kikundi hicyo kwa hivyo..

(Sauti ya Farhan)

Mjumbe huyo maalum atazungumza na Rais mteule Muhammadu Buhari kesho kuhusu jinsi jamii ya kimataifa inaweza kutoa msaada kuwezesha kuachiliwa huru kwa watoto hao. Halikadhalika wajadili usalama shuleni wakati huu ambapo watoto Milioni 10 Nigeria hawaendi shule.”

Bwana Brown amesema kwa kuweka mazingira ambamo kwayo jamii na watoto hawana hofu, itakuwa rahisi watoto kwenda shule na kujifunza.