Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Itifaki ilikiukwa katika uchunguzi Jamhuri ya Afrika ya Kati: Ban

Itifaki ilikiukwa katika uchunguzi Jamhuri ya Afrika ya Kati: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiaf Ban Ki-moon amesema itifaki ilikiukwa katika  mchakato wa upelelezi kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kingono na ukatili dhidi ya watoto uliofanywa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu mjini Bangui.

Taarifa ya Katibu Mkuu kupitia ofisi ya msemaji wake imesema kuwa upelelezi huo uliofanywa mwaka 2014 uliwahusisha maafisa wa jeshi la Ufaransa kuelekea kuanzishwa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Ban amesema kuwa matokeo ya uchunguzi huo yalitolewa kwenye sherehe ya nje ya ofisi katikati ya mwezi Julai mwaka 2014 yakiwa hayajahaririwa ambapo yalitaja majina ya waathiriwa, mashahidi na wachunguzi.

Amesema kuwa toleo hilo lisilohaririwa lilitolewa kwa ruhusa tu ya mfanyakazi hata kabla ya kuwasilishwa kwa  uongozi wa juu wa ofisi ya kamishna mkuu wa haki za binadamu OHCHR jambo alilosema ni uvunjifu wa itifaki ambao kama ijilikanavyo na maafisa wa OHCHR inapaswa kuondolewa kwa taarifa zinazoweza kuhatarisha waathiriwa, mashahidi na wachunguzi.

Bwana Ban pia amesema kuwa kuna uchunguzi wa ndani kuhusu namna ya kushughulikia suala hili kupitia OHCHR ikiwamo suala la namna siri za ukusanyaji wa taarifa za awali ulivyofikishwa kwa wadau nje na ikiwa majina ya waathirika, mashahidi na wachunguzi uliwafikia kama sehemu ya uchunguzi. Amesema mmoja wa wafanyakazi amepewa likizo yenye malipo kufuatia uchunguzi ambao haujakamilika.

Amesema tathimini ya awali inaoyesha kuwa uendeshaji wa namna hiyo wa uchunguzi hausababaishi upazaji wa sauti.