Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNWTO kusaidia kukwamua sekta ya utalii Kenya:

UNWTO kusaidia kukwamua sekta ya utalii Kenya:

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utalii, UNWTO limeelezea mshikamnao wake na serikali na wananchi wa Kenya katika harakati zake za kukwamua sekta ya utalii nchini humo wakati huu ambao nchi hiyo imekumbwa na matukio ya ugaidi.

Katibu Mtendaji wa UNWTO Taleb Rifai amesema hayo wakati wa ziara yake nchini humo ambapo alikuwa na mazungumzo na viongozi mbali mbali akiwemo Rais Uhuru Kenyatta.

Rais Kenyatta katika mazungumzo hayo alieleza kuwa wanaendelea kuchagiza sekta hiyo ya utalii hata wakati huu majaribu akisema suala la ugaidi si la Kenya pekee bali ni la kimataifa kwa hivyo wataimarisha pia ushirikiano na nchi jirani.

Kufuatia kauli hiyo Bwana Rifai amesema ulimwengu una heshima kubwa kwa Kenya kama sekta ya utalii duniani inavyoheshimu nchi hiyo na hivyo akatoa hakikisho kuwa UNWTO itatekeleza wajibu wake ili kurejesha imani kwa sekta ya utalii ya nchi hiyo.