Somalia yasafirisha mifugo milioni 5 kwenda Ghuba mwaka jana:FAO

29 Aprili 2015

Somalia imevunja rekodi na kusafirisha mifugo milioni tano katika soko la ghuba mwaka 2014, kutokana na uwekezaji mkubwa wkatika kupambana na magonjwa ya mifugo limesema shirika la chakula na kilimo FAO.

Kwa mujibu wa shirika hilo hii ni idadi kubwa kabisa ya mifugo hai kusafirishwa kutoka Somalia kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita. Baada ya kuondolewa marufuku ya miaka 9 ya kuingiza mifugo, sasa Somalia iko katika nafasi ya kuimarisha uchumi na maisha ya mamilioni ya wamiliki na wafugaji nchini kote.

Rudi van aaken ni afisa wa FAO ofisi ya Somalia iliyopo Nairobi Kenya anaeleza Zaidi mabadiliko katika sekta hiyo ya mifugo ya Somalia na inamaanisha nini kwa taifa hilo.

(SAUTI YA RUDI VAN AAKEN)

"Takriban asilimia 42 ya pato la kitaifa ni kutoka sekta ya mifugo, ambayo inaajiri watu wengi nchini Somalia. Asilimia 80 ya familia wanategemea sekta hii na pia katika sekta zinazoingiliana na sekta hii ikiwemo usafiri, au huduma za afya ya mifugo na katika matumizi ya bidhaa zitokanazo na mifugo ikiwemo ngozi na uchongaji wa mifupa ambazo FAO inazisaidia ili kuwezesha biashara bora."

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter