Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vurugu sio suluhu ya mgogoro wa Burundi:IPU

Vurugu sio suluhu ya mgogoro wa Burundi:IPU

Muungano wa mabunge duniani IPU ukilaani vurugu nchini Burundi ambazo zimeshasababisha vifo vya waandamanaji kadhaa katika purukushani na polisi siku chache zilizopita, umezitaka pande zote nchini humo kujizuia na kuepuka umwagaji damu zaidi. Grace Kaneiya na taarifa zaidi

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

IPU inazidi kutiwa hofu na ongezeko la ghasia kufuatia maandamano mitaani dhidi ya uamuzi wa kumtangaza Rais Pierre Nkurunziza  kutaka kugombea Urais awamu ya tatu na pia kusambaza polisi mitaani kukabiliana na waandamanaji.

Waandamanaji wanaomiminika mitaani ni wengi zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo mwaka 2005 , wakati rais Nkurunziza alipoanza muhula wa kwanza ya utawala wake.

IPU pia imetoa wito wa kuwepo kwa Amani , uwazi na usawa katika mchakato wa uchaguzi ili kuhakikisha Burundi inaendelea katika njia ya demokrasia. Uchaguzi wa bunge unatarajiwa kufanyika mwezi Mai ukifatiwa na wa Rais hapo mwezi Juni.