Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simulizi ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi alivyoshambuliwa na kukatwa kiungo

Simulizi ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi alivyoshambuliwa na kukatwa kiungo

Nchini Tanzania, watu 35,000 ni wana ulemavu wa ngozi au albino. Ni hali ya ngozi inayosababisha madhara mbali mbali ikiwemo kutoona vizuri na matatizo ya ngozi hadi saratani.Lakini kutokana na imani za kishirikina, hali hiyo imedaiwa kuhusishwa na biashara ikidaiwa kuwa kiungo cha mlemavu wa ngozi kinaweza kuongeza utajiri wa mtu.

Tangu mwaka 2000, mashambulizi zaidi ya 150 yalitokea dhidi ya watu wenye ulemavu huo na watu 75 wameuawa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Baada ya kupungua tangu mwaka 2007, mashambulizi hayo yameanza kutokea tena, watu wawili wakiuawa tangu mwanzo wa mwaka huu, huku Umoja wa Mataifa ukijaribu kuelimisha jamii na kuchukua hatua kupitia maeneo matatu muhimu : kulinda, kuzuia na kushtaki.

Je ni madhila gani wanapitia albino na kulikoni ? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.