Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na kufanya mazungumzo na Papa Francis

Ban akutana na kufanya mazungumzo na Papa Francis

Akiwa mjini Roma Italia kuhudhuria kongamano kuhusu kulinda dunia na utu wa mwanadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon amekutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa kanisa katoloki duniani papa Francis ambapo viongozi hao pamoja na mambo mengine wamejadili kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

Bwana Ban amemueleza Papa Francis kuwa anautarajia waraka kutoka kwa kiongozi huyo wa kanisa katoliki juu ya mabadiliko ya tabia nchi ambao amesema utakuwa ni sauti ya maadili kuhusu suala hilo.

Katibu Mkuu pia amemuarifu Papa kuhusu ziara yake ya leo kujionea operesheni za uokozi wa wahamiajai na wasaka hifadhi kwenye bahari ya Mediterranean. Kadhalika viongozi hao wamejadili ujumuishwaji wa kijamii, biashara haramu ya kusafirisha binadamu na ain azote za utumwa .

Awali akionge katika ufunguzi wa kaongamano kuhusu kulinda dunia na utu wa mwanadamu Ban amesisitiza kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

(SAUTI BAN)

"Mabadiliko ya tabia nchi yanatuiathiri sisi sote lakini si kwa usawa. Wanaoathiriwa sana ni wale ambao hawasababishi zaidi mabadiliko hayo, hawa ni maskini na walio katika mazingira hatarishi zaidi katika jamii. Hii ni kwasababau hawana njia na mbinu na rasilimali za kukabiliana na mabadiliko haya."