Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutarajiwa kushuka kwa uzalishaji wa mahindi kusini mwa Afrika kwaleta hofu ya usalama wa chakula:FAO

Kutarajiwa kushuka kwa uzalishaji wa mahindi kusini mwa Afrika kwaleta hofu ya usalama wa chakula:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO , Jumanne limeonya kwamba mavuno ya mahindi Kusini mwa Afrika yanatarajiwa kushuka mwaka huu kwa takriban asilimi 26 ukilinganisha na mwaka 2014.

Kwa mujibu wa FAO hii ni hali ambayo itasababisha kupanda kwa bei ya chakula na kutia dosari katika hali ya sasa ya usalama wa chakula.

Jonathan Pound is ni mchumi katika shirika la FAO mjini Roma , anaelezea anaelezea yaliyobainika katika ripoti mpya ya FAO.

(SAUTI YA JONATHAN POUND)

"Kufuatia kushuka kwa uzalishaji mwaka huu tunatarajia uagizaji mkubwa wa bidhaa kutoka nje kwenye  katika maeneo mengi ya ukanda huo ikiwemo Afrika Kusini na zaidi  Zimbabwe inatarajiwa kuagiza zaidi. Kuna mataifa mengi ambayo yataagiza bidhaa nje ili kukidhi mahitaji yao ya ndani . Hata hivyo  kutokana na  uwepo wa  bidhaa nyingi kutokana na mavuno mengi  katika nchi zingine barani humo, bei katika nchi nyingine ni za chini ikilinganishwa na mwaka jana na hii itasaidia upatikanaji wa mahindi kwa kaya zilizo hatarini zaidi."