Timu ya dharura ya IOM yawasali Nepal kutoa msaada:

28 Aprili 2015

Wafanyakazi wa dharura wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM , wamewasili Nepal kusaidia serikali na washirika wa kutoa misaada ya kibinadamu kukabiliana na athari za tetemeko la wiki iliyopita.

Asubuhi ya leo Jumanne timu hiyo imeshakutana na maafisa wa serikali ambao wameifahamisha idadi ya waliopoteza maisha ni Zaidi ya 3300, Zaidi ya 6000 wamejeruhiwa huku wengine Zaidi ya milioni 8 kuathirika na tetemeko hilo, ingawa taarifa ambazo hazijathibitika zinasema waliokufa ni Zaidi ya 4000 na kujeruhiwa ni Zaidi ya 8000. Joel Milman ni msemaji wa IOM

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter