Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UN Women yataka mabadiliko ya kiuchumi na kutimiza ndoto za haki na usawa:

Ripoti ya UN Women yataka mabadiliko ya kiuchumi na kutimiza ndoto za haki na usawa:

Ripoti kubwa na muhimu ya kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women, imetolewa leo katika maeneo saba duniani , ikiwaleta pamoja wanaharakati wa haki za binadamu na watunga sera za kiuchumi , ili kutoa wito wa kufanya mabadiliko katika ajenda ya sera za dunia ambazo zitabadili uchumi na kufanya ndoto za haki za wanawake na usawa kutimia.

Ripoti hiyo inaangalia kwa kina nini kitakachofanywa katika Nyanja ya uchumi ambacho kitaonekana kweli kinaleta mabadiliko kwa wanawake kwa ajili ya faida kwa wote.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo hatua zilizopigwa hadi sasa ni dhahiri kwamba ajenda mbadala ya kiuchumi inayotajwa , sio tuu italeta usawa katika jamii bali pia itaunda sekta mpya za ajira hususani katika Nyanja ya kiuchumi.

Ripoti hiyo imechapishwa wakati jumuiya ya kimataifa inaungana pamoja kuleta mabadiliko katika ajenda mpya ya maendeleo endelevu, miaka 20 baada ya mkutano wa kihistoria wa wanawake uliofanyika mjini Beijing China ambao uliweka ajenda muhimu za kuimarisha usawa wa kijinsia.