UNHCR yaonya mzozo wa CAR wasahaulika

UNHCR yaonya mzozo wa CAR wasahaulika

Takribani watu 900,000 kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, wamelazimika kuhama makwao tangu mwanzo wa mapigano disemba 2013 na kwa ujumla ni watu milioni 2.7 wanahitaji msaada wa kibinadamu, lakini mpango wa usaidizi umefadhiliwa kwa kiwango cha asilimia 14 tu.

Akizungumza leo na waandishi wa habari mjini Geneva, Claire Bourgeois ambaye ni mratibu wa kibinadamu nchini CAR amesema kuna matumaini ya kumalizika wa mzozo, wakati ambapo kongamano la maridhiano la Bangui linatarajiwa kuanza wiki ijayo na uchaguzi wa rais mwezi wa Agosti.

Kwenye mazingira hayo ya kisiasa, ambayo yameanza kuleta hali ya utulivu na usalama, usaidizi wa kibinadamu unapaswa kwenda sambamba, Lakini hata hivyo bado kuna mzozo wa kibinadamu hapa, nazumgumzia maeneo ya mapigano ambapo tunaona mapigano zaidi, watu wengi zaidi wanalazimika kuhama makwao, wengind wanajaribu kurudi makwao lakini wanapaswa kurudi kambini” 

Mahitaji ya kifedha kwa ajili ya mzozo wa CAR ni takriban dola milioni 600.