Skip to main content

Mashirika ya UM yaungana na wadau wengine kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko Nepal

Mashirika ya UM yaungana na wadau wengine kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko Nepal

Mashirika mbalimbali ya Umoja wa mataifa ymaeungana na wadau wengine kutoa misaada ya kibinadamu inayohitajiwa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi na maporomoko ya theluji nchini Nepal. Taarifa ya Grace Kaneiya inafafanua.

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Mashirika hayo likiwemo la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la afya WHO, la mpango wa chakula WFP  na la elimu sayansi na utamaduni UNESCO yamekuwa msitari wa mbele kupeleka misaada mbalimbali ya kibinadamu inatohitajika kwa maelfu na maelfu ya watu walioathirika  na tetemeko la Jumamosi ambalo hadi sasa limekatili maisha ya Zaidi ya watu 3000 na kujeruhi wengine wengi.

UNHCR kwa upande wake Jumatatu ya leo linapeleka mifuo ya plastiki 11,000 na kandili 4000  zinazotumia mwanga wa jua katika wilaya za Ramechnap, Okhaldhunga na Sinduli kwa ombi maalumu la serikali ya Nepal na baadaye watapeleka mifuko mingine 8000 na kandili 4000 mjini Kathmandu.

Shirika la afya WHO  hadi sasa limeshagawa vifaa vya dharura vya kwa Zaidi ya watu 40,000 vitakavyoweza kuwasaidia kwa miezi mitatu na linapeleka timu ya wataalamu wa afya 10. Limesema mahitaji ya haraka ni kuhifadhi waliopoteza maisha na kutibu waliojeruhiwa. Pia shirika hilo limetoa dola 175,000 kwa wizara ya afya ya nchi hiyo.

Nalo shirika la WFP ambalo linakusanya msaada wa chakula na kusafirisha kwa waathirika kesho Jumanne litapeleka biskuti za kutia nguvu , huku timu yake inayohusika na mipango na huduma ya dharuka imewasili Kathmandu.

Mbali ya vifo na majeruhi tetemeko hilo na maporomoko vimesambaratisha vibaya nyumba, na majengo ya kihistoria na urithi nchini humo  kama anavyoeleza mkuu wa ofisi ya UNESCO nchini Nepal Christian Manhart

(CLIP YA CHRISTIAN MAHART)

Hali ya maeneo ya urithi ni ya kusikitisha katika bonde la Kathmandu, hatujamaliza utafiti kuhusu maeneo yote kwa hiyo hatuna uhakika kuhusu maeneo saba ya urithi Kathmandu ambako kumekuwa na uharibifu mkubwa hususan Durbar square ambako karibu misikiti yote imeharibiwa"