Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timu ya dharura ya IOM yawasili Nepal kutoa msaada

Timu ya dharura ya IOM yawasili Nepal kutoa msaada

Wafayankazi wa dharura wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wamewasili nchini Nepal kuisaidia serikali na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu kukabiliana na athari za tetemeko la aridhi la tarehe 25 ambalo limesababisha madhara makubwa na kupoteza maisha ya watu wengi.

Hadi sasa watu Zaidi ya 3600 wamefariki dunia huku takwimu kamili kutoka katika eneo ambalo lilikuwa kitovu cha tetemeko hilo kilometa 80 nje kidogo ya mji mkuu Kathmandu hazijapatikana.

Maelfu ya watu wamejeruhiwa huku hospitali na vituo vya afya vikilemewa, na majengo mengi ya kihistoria, nyumba za kuishi pia zimesambaratishwa vibaya na watu wengi inasemekana wamenasa katika kifusi.

Pia taarifa zinasema baadhi ya watu waliokuwa wakipanda mlima Eeverest wameuawa kutokana na maporomoko ya theluji na matopo yaliyosababishwa na tetemeko hilo.