Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon asikitishwa na tetemeko la ardhi Nepal

Ban Ki-moon asikitishwa na tetemeko la ardhi Nepal

Katika taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amenukuliwa akisema maisha mengi yamepotezwa na urithi wa utamaduni wa Nepal pia umeharibika kwa kiasi kikubwa, huku ripoti zikiendelea kufika na idadi ya vifo kuzidi kuongezeka.

Bwana Ban ametuma salamu zake za rambirambi kwa serikali ya Nepal, familia na marafiki za wahanga, akishukuru pia watu waliojitolea mapema ili kuokoa maisha.

Umoja wa Mataifa unaisaidia serikali ya Nepal ili kuratibu operesheni wa kuokoa watu na kuanda usaidizi wa dharura.