Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon aeleza wasiwasi wake juu ya mashambulizi dhidi ya MINUSMA Mali

Ban Ki-moon aeleza wasiwasi wake juu ya mashambulizi dhidi ya MINUSMA Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya mashumbulizi yanayolenga Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA na wanaoshirikiana na MINUSMA yaliyoua raia 5, na kujeruhi watu 29 tangu wiki iliyopita, wakiwemo walinda amani 16.

Mashambulizi haya yametokea katika maeneo ya kaskazini mwa Mali, yakiwa ni mabomu yaliyotegwa barabarani au waasi walioshambulia msafara wa magari.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Katibu Mkuu amenukuliwa akisema mashambulizi dhidi ya raia au walinda amani ni ukiukaji wa sheria za kimataifa, akiomba kwamba wale waliotekeleza mashambulizi hayo wapelekwe mbele ya sheria.

Bwana Ban ameongeza kwamba mashambulizi hao yanaonyesha umuhimu wa kupata suluhu ya kudumu nchini humo.

Aidha amepeleka rambirambi zake kwa familia za wahanga na kuwatakia nafuu waliojeruhiwa