Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wanaokimbia Yemen kwende Pembe ya Afrika wafikia 10,000 IOM

Wahamiaji wanaokimbia Yemen kwende Pembe ya Afrika wafikia 10,000 IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema linaendelea kutoa msaada wa kibinadamu kwa wahamiaji, wakimbizi na raia wa nchi ya tatu wanaowasili Pembe ya Afrika wakikimbia machafuko nchini Yemen.

Kwa mujibu wa shirika hilo watu waliowasili wiki hii pekee pembe ya Afrika ikiwemo Djibouti, Somaliland na Puntland ni 10,263.

Djibouti ndio inayopokea kundi kubwa la watu na idadi imeongezeka na kufikia 8,344 wiki hii, na asilimia 60 ya watu hao ni wa taiafa la tatu wanaohitaji msaada wa kurejea nyumbani.