Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo ya surua na polio yaanza katika nchi zilizoathirika na ebola na Mashariki ya Kati:UNICEF

Chanjo ya surua na polio yaanza katika nchi zilizoathirika na ebola na Mashariki ya Kati:UNICEF

Wiki ya chanjo duniani imeanza leo kwa lengo la kuziba pengo lililopo kwa majonjwa mbalimbali na itamalizika April 30. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya magonjwa yanayozuilika kama surua na polio imeanza katika nchi mbalimbali ikiwemo Yemen, Syria na mataifa matatu ya Afrika ya Magharibi yaliyoathirika vibaya na homa ya ebola limetangaza Ijumaa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Kwa mujibu wa shirika hilo hii ni mara ya kwanza kampeni hiyo ya chanjo inawezekana tangu kuzuka kwa ebola katika nchi ya Guinea,Sierra Leone na Liberia.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa mataifa msemaji wa UNICEF Christophe Boulierac amesema changamoto ya kuwalinda watoto milioni 3 imekuwa ngumu Zaidi kutokana na kutojiamini kwa wahudumu wa afya kulikosababishwa na ebola.

(SAUTI YA CHRISTOPHE BOULIERAC)

"Kwa wastani uwepo wa Ebola unasababisha maambukizi mawili mapya huku kisa kimoja cha surua kikisababisha maambukizi ya hadi visa 18 miongoni mwa watu walioko katika hatari zaidi na njia muafaka ya kukabiliana na mlipuko mkubwa wa surua ni kurejesha huduma ya kutoa chanjo kwa utaratibu ikizingatia utafiti unaoendelea wa hali ya ebola katika mataifa haya matatu."