Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati dhidi ya chuki na ghasia lazima ziende na wakati: Deng

Harakati dhidi ya chuki na ghasia lazima ziende na wakati: Deng

Mitandao ya kijamii na intaneti pamoja na manufaa yake, kwingineko inatumia vibaya kueneza chuki na ghasia, amesema Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari  Adama Dieng huko Fez nchini Morocco kando mwa mkutano kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika kuzuia uchochezi unaoweza kusababisha vitendo vya ukatili.

Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa Bwana Deng ametolea mfano vikundi vya kigaidi ambavyo vinatumia mitandao ya kijamii kushawishi watu kujiunga nao kwa misingi ya dini na hivyo kwenye mkutano huo wa siku mbili wanajadiliana na viongozi wa dini ili..

(Sauti ya Deng)

"Viongozi hawa wa kidini watajadili kile wanachopaswa kufanya, wanachopaswa kusema pindi maneno ya kichochezi au chuki yanaposemwa kwenye jamii zao au hata katika jamii nyingine.”

Amesema jitihada kupitia mikutano kama huo wa Fez ni lazima ziendelee kwani nyaraka mbali mbali zilizopo za kuzuia watu kujenga chuki kwa misingi ya dini hazijaweza kuleta matunda na akatoa mfano jinsi viongozi wa dini wanavyobadilishana uzoefu wa kile wanachofanya makwao kujenga maelewano.

(Sauti ya Deng)

"Mmoja wa washiriki ambaye ni mchungaji kutoka Nigeria ambaye kwa miaka takribani 20 jamii yake ya kiprotestanti na jamii ya kiislamu walikuwa katika mzozo na kukaribia kuuana, hata mwenyewe alipoteza mkono wake, lakini hatimaye aliwezesha amani.”

Matarajio mwishoni mwa mkutano huo pamoja na mambo mengine ni kuunda mtandao wa viongozi wa kidini watakaokuwa wajumbe wa amani kwenye jamii zao.